The House of Favourite Newspapers

Video: CCM Yapita Bila Kupingwa Vijiji 6, 248 Uchaguzi Serikali Za Mitaa 2019

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo leo Novemba 10, 2019 amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepita bila kupingwa katika vijiji 6,248 kati ya 12,319 mitaa 1,169 kati ya 4,263 na vitongoji 37,505 kati ya 64,384.
“CCM wamepita bila kupingwa maeneo mbalimbali kwakuwa hakukuwa na Mgombea wa Chama kingine, ni wao pekee ndio walichukua na kurudisha fomu, upande wa Wenyeviti wa Vijiji wa CCM waliopitishwa bila kupingwa ni 6,248 kati ya 12,319 sawa na 51%.

“Ofisi yangu imejitahidi sana kufanya kazi kwa weledi mkubwa tukijua wazi kuwa Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa ni muhimu, Watumishi wa Wizara ya TAMISEMI hatulali, tunapambana na Uchaguzi huu”  amesmema Waziri Selemani Jafo.

Comments are closed.