The House of Favourite Newspapers

Video: Dk Shika Ala Shavu la Nguvu Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Sokabet

0

Dk. Louis Shika amekula shavu la nguvu baada ya kusaini mkataba na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Sokabet ambapo tayari anaonekana kwenye tangazo la kampuni hiyo akiwa amevaa jezi zenye jina lake na kampuni hiyo ya michezo.

Dk. Shika ambaye amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuibuka mshindi kwenye mnada wa nyumba za kifahari za bilionea Lugumi na baadaye kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba hizo, anasikika kwenye tangazo hilo akijinadi kwamba wakati anasubiri mabilioni yake, ameamua kubeti ili ajishindie shilingi milioni 100.

Hivi karibuni, Dk. Shika alilipa kiwango cha dola 100 za Kimarekani (sawa na shilingi 220,000), kama bima ili aweze kutumiwa mabilioni yake kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa ununuzi wa nyumba hizo.

 

Leave A Reply