The House of Favourite Newspapers

Video: Dkt. Louis Shika Asimulia Maisha Yake – 2

0
…Akiwa na Sifael Paul na Mhariri Mwandamizi wa gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kushoto) wakati wa mahojiano kuhusu yaliyompata.

BAADA ya kuwatoroka watekaji wangu, nikakutana na watu walionisaidia na kunipeleka polisi ambao walinipeleka hospitali.  Polisi walifanya kila juhudi kuitafuta nyumba niliyokuwa nimetekwa kwa kunitembeza sehemu nyingi hadi tulivyoipata na kuitambua  lakini hapakuwa na mtu wa kumkamata.

 

Polisi waliniuliza iwapo kulikuwa na mtu niliyekuwa namtilia shaka kuhusu utekaji huo, niliwambia nilikuwa na shaka na mhasibu wangu wa kike ambaye alikuwa ana mawasiliano na watu ambao nilikuwa siwajui.


Baada ya polisi kumhoji kwa mateso, alikubali na hatimaye alifungwa miaka 15 jela baada ya kufikishwa mahakamani.  Wale wenzake wanne alioshirikiana hao hadi leo sijajua kama walikamatwa au la.

 

Nilitibiwa hospitali kwa muda hadi nilipopata nafuu, ubalozi wa Marekani ukanisafirisha kwenda Uholanzi ambako nilipandishwa  ndege ya Kenya Airways hadi Nairobi hatimaye Tanzania nilikofika Januari Mosi, 2005.

 

Nilikuwa na wasiwasi na Warusi kunifuata hapa Tanzania, jambo ambalo ni kawaida yao kuwafuata maadui zao hadi wawaue, hivyo nikaenda Madrid, Hispania, kuwakimbia.  Nilikaa huko hadi niliporidhika kwamba usalama wangu ulikuwa angalau katika hakika.

Nikarejea nchini Novemba 20, 2013, sikutoka tena zaidi ya kwenda Kenya mwaka 2014 kutokana na kupata barua iliyoniita kwenda kwenye uteuzi wa balozi wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR).

 

Pia nilipata wito kutoka Umoja wa Mataifa kutoka kwa Katibu Mkuu, Antonio Gutterezi, kupitia shirika la Organisation for Economic Cooperation Development  (OECD), lakini sikutaka kujiunga nalo.

 

Kuhusu fedha yangu iliyokuwa Urusi kwenye kampuni yangu, niliomba isambazwe duniani ili kukwepa majanga yanayoweza kuipata ikiwekwa sehemu moja.  Hivyo, ilisambazwa sehemu mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na Israel palikowekwa fedha nyingi  zaidi kwenye First International Bank of Israel.

 

Kuhusu mnada, nilizitaka nyumba zilizokuwa zinauzwa kwa ajili ya wafanyakazi wangu ambao wangekuja hapa nchini.  Tatizo sikuwa na fedha taslimu ya kulipa moja kwa moja baada ya mnada, jambo lililonisababishia matatizo, kwani waendesha mnada walitaka nilipe taslimu.

 

Matokeo yake nilikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi Selander na hatimaye kituo kikuu jijini Dar es Salaam.

Simulizi hii ya kusisimua inaendelea kesho Global TV Online, hivyo usikose kuiona.

NA WALUSANGA NDAKI | GLOBAL PUBLISHERS

Dkt. Louis Shika Asimulia Maisha Yake (Video)

Leave A Reply