The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Harmorapa Awachana WCB, Adai Anawazidi kwa Mashabiki, Aboronga Kiingereza

0

RAPA anayekuja kwa kasi kwenye game ya Bongo, Harmorapa mwenyewe anajiita ‘Kiboko ya Mabishoo’, amefanya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness Malinzi, ‘Diva’ ambapo katika mwendelezo wa mahojiano hayo, mkali huyo amezungumza mambo mbalimbali, huku akitamba kuwafunika WCB kwa wingi mashabiki wakati huo huo akiboronga vibaya Lugha ya Kiingereza.

Harmorapa amewachana WCB kwamba hawezi kufanya Collabo na wasanii kutoka WCB kwa sababu hawana cha kumuongezea, akachana pia kwamba yeye ana mashabiki wengi kuliko WCB.

Kubwa lililowafurahisha wengi, ni jinsi alivyokuwa akibabaika anapoulizwa maswali ya Kiingereza na amekiri kwamba ni kweli aliwahi kusema yeye ni stron gwoman lakini alichapia kwa bahati mbaya.

Harmorapa amefungukia mambo mbalimbali ya uhusiano wake wa kimapenzi ambapo amesema hajawahi kupenda kwa dhati kutoka ndani ya moyo wake.

VIDEO: Bofya Kuzikiliza Alichokisema Harmorapa

Leave A Reply