The House of Favourite Newspapers

Video: Highlights Za Premier League Wikiendi Hii Hizi Hapa…

0

Premier League iliendelea wikiendi hii, Jumamosi ya Septemba 10, 2016 Manchester United iliambulia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Bao la Man United lilifungwa na Zlatan Ibrahimovic katika dakika ya 42, wakati mabao ya Man City yaliwekwa wavuni na Kevin De Bruyne dakika ya 15 na Kelechi Iheanacho dakika ya 36, video ya kilichotokea katika mchezo huo hii hapa…

Liverpool ilitoa kichapo kikali kwa mabingwa watetezi Leicester City mabao 4-1 wafungaji wa Liverpool walikuwa ni Roberto Firmino, Sadio Mane, Adam Lallana na Firmino tena wakati lile la mabingwa hao liliwekwa wavuni na Jamie Vardy kwenye Uwanja wa Anfield.

Shuhudia mabao hayo hapa…

Arsenal ilipata ushindi katika dakika za majeruhi kwa kuifunga Southampton mabao 2-1, wafungaji wa Arsenal ni Laurent Koscielny dakika ya 29 na Santiago Cazorla kwa njia ya penalti katika dakika ya 94 baada ya mwamuzi wa akiba kuongeza dakika tano wakati 90 zilipomalizika. Bao la wapinzani liliwekwa wavuni na kipa wa Arsenal, Petr Cech ambaye alijifunga katika dakika ya 18.

Check mabao hayo hapa…

Stoke City ilipata kipigo cha mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Britannia ilipokutana na Tottenham Hotspur, wafungaji wakiwa ni Heung-Min Son (41 na 56), Bamidele Alli (59) na Harry Kane (70).

Video ya mabao hayo hii hapa..

Leave A Reply