VIDEO: Historia ya Watanzania Waliopigana Vita ya Dunia!

VIJANA kumi na tano elfu kutoka Tanganyika, walikamatwa kwa nguvu kwenda kupigana Vita ya Pili ya Dunia ili kuikomboa Uingereza dhidi ya kiongozi wa Ujerumani, Adolf Hitler.  Vijana hao wakamshinda Hitler, Waingereza wakapiga vigelegele, na hatimaye vijana hao wa kazi wakarudi nyumbani na majina ya kishujaa.  Sasa ni wazee, hawana nguvu tena, hawaoni vizuri, hawasikii vizuri, hawana kumbukumbu nzuri, hawana meno, wengi wamekufa na huzuni moyoni.

Wengi wao wakiwa na hasira kichwani, ukata mifukoni, wamebaki ‘vijana’ 400 kati ya 13,000 waliorudi, mwenye umri mdogo ana miaka 92, wengi hatujui walipo kwa sababu hatuijui historia yetu.  Uingereza haijui walipo kwa sababu shukurani ya punda ni mateke.

 

Wakati wanasakwa kwenda vitani aliyejifanya kukaidi alitupwa jela miezi sita na viboko juu, alipotoka jela aliulizwa kuchagua kwenda vitani au kurudi jela tena miezi sita.  Wote walichagua kwenda vitani kupigana,  vita ambavyo havikuwahusu.

 

Tatizo la Wazungu ni kwamba wao wakizinguana wanasema ni vita ya dunia na kutulazimisha tukawasaidie.  Sisi tukizinguana wanasema ni vita vya ukabila na kuja kutuuzia silaha tuuane,  wao wachume kwa sababu kwenye vurugu pana ulaji.

 


Loading...

Toa comment