Video: Hoja ya kumuondoa Madarakani Naibu wa Rais wa Kenya yaanza kujadiliwa bungeni

BUNGE la Kitaifa nchini Kenya leo Oktoba 8, 2024 limeanza kujadili hoja ya kuondolewa madarakani kwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua.
Hatua hii ni baada ya Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse kuwasilisha sababu 11 kupitia hoja ya kutaka kumuondoa madarakani mnamo tarehe Septemba 26, 2024.
Naibu Rais wa Kenya Geoffrey Rigathi Gachagua anatarajiwa kufika mbele ya Bunge la kitaifa mwendo wa saa kumi na moja jioni ya Jumanne Octoa 8 ili kujitetea dhidi ya mashtaka 11 yaliyowasilishwa.
Baada ya saa mbili za kujieleza na kujibu maswali, Gachagua ataondoka bungeni na kuwaacha wabunge wakijadili majibu yake, kwa muda.
Usiku wa leo, Spika Wetangula anatarajiwa kutangaza rasmi kwamba kikao maalum cha bunge kiko tayari kupigia kura hoja hiyo ya kumuondoa kazini Naibu Rais Gachagua.
Atawaomba viranja wa bunge kupiga kengele ya kuidhinisha kura hiyo kupigwa.
Kura huweza kupigwa kwa njia ya siri kupitia mashine za Kompyuta wanapoketi Bungeni. Kila mbunge ana kadi maalum yenye taarifa zae muhimu ambayo ataitumia kupiga kura , kisha matkeo yatangzwe kwenye Bunge kupitia (screen) iliyopo bungeni.