Video: JPM Akabidhi Tausi Marais Wastaafu Dodoma

RAIS John Magufuli leo Mei 30, 2020, amewakabidhi ndege 25 aina ya tausi kila mmoja, marais wa awamu zilizopita kwa ajili ya kupamba bustani za makazi yao.

Marais hao ni Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete na marehemu Mwalimu Julius Nyerere ambapo zawadi hiyo ilipokelewa na mkewe (mjane), Mama Maria Nyerere.
Tukio hilo limefanyika makao makuu ya nchi jijini Dodoma wakati wa sherehe ya kuzindua ujenzi wa ofisi za ikulu ambapo alisema amefanya juhudi kubwa katika kuwatunza tausi 403 aliowakuta ambapo hadi sasa kuna tausi 2,260 katika bustani za Ikulu ya Dodoma na Dar es Salaam.
Magufuli alisema aliongeza idadi ya ndege hao wenye kuvutia kwa kununua mashine ya kusaidia kutotolea mayai ya ndege yao, jambo lililosababisha kuongezeka kwake, tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, alimshukuru Magufuli kwa kuwatunuku zawadi hiyo.



Tazama video ya chini kwa habari zaidi.

