The House of Favourite Newspapers

VIDEO: JUX Afunguka ISHU ya Kutoka Kimapenzi RUBY

Mwimbaji wa Bongo Fleva, Juma Jux akifanya mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia kutoka +255 Global Radio.

MWIMBAJI wa Bongo Fleva, Juma Jux, leo Novemba 11, 2019 amefanya mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia kutoka +255 Global Radio kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni.

…Mahojiano yakiendelea.

Akifanya mahojiano katika kipindi hicho ameongelea ishu yake na msanii wa Bongo Fleva, Ruby ameyasema haya;-

“Nimeona, nimesikia sababu kilikuwa ni kitu ambacho kinaenda viral sana, kiukweli sikutaka kufanya chochote, nilitaka kuona sababu ni nini na kwa nini inatokea hivi; ila mtu kama Ruby ni msanii ambaye sikuwahi hata kuwa naye katika mazoea, ila ni mtu ninayemfahamu toka hata kabla hajatoka, nilimkuta kwa Bob mara ya kwanza alikuwa anaimba wimbo wangu wa sisikii,”.

 “Nilimwambia napenda anavyoimba, Sijawahi kuwa na mahusiano na Ruby. Nilitamani kumshirikisha katika kazi yangu kutokana na sauti yake, Ruby she’s the talented artist, tulimalizana kwenye kazi tu. There is nothing,” Alisema Jux

Nilikuwa sijafikria kutoa album kwa sababu ya mindset ya nyuma kuwa Album haziuzi tena, ila kuna sehemu ukienda watu wanakuuliza kuhusu album yako, Utaona Album ni certificate kwa msanii kujua kama kweli umekua, The Love Album imekuwa na records nzuri “Duniani Album yangu ni ya pili ya mapenzi kwenye Mtandao wa Audiomack baada ya Album ya Tory Lanez, na kwenye mtandao wa Boomplay ni namba 1 kwa Afrika mashariki.” Alisema Jux

Comments are closed.