The House of Favourite Newspapers
gunners X

VIDEO: KESI YA BABU TALE YAAHIRISHWA, ARUDISHWA MAHABUSU

Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde akiwa na mawakili wake leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, leo amefikishwa katika Mahakama Kuu jijini Dar ambako baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo kesi imeahirishwa na Babu Tale kurudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam mpaka hakimu aliyetoa amri ya kukamatwa kwake atakaporejea.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ (katikati aliyekaa) akiwa na wakili wake na ndugu zake mahakamani hapo.

Mahakama hiyo pia leo ilitoa fursa kwa pande mbili zinazohusika katika kesi hiyo kujadiliana lakini baada ya majadiliano hayo pande zote zilirudisha majibu kwa hakimu kwamba hazikufikia maelewano yoyote.  Hivyo msajiri wa Mahakama Kuu alichukua uamuzi wa kuiahirisha tena kesi hiyo.

…Wakiendelea kuongea.

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA DENIS MTIMA  | GPL

Comments are closed.