The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Kocha Vita Aipa Siri Yanga

KOCHA mkuu wa klabu As Vita Club ya DR Congo, Florent Ibenge anaamini Yanga itatwaa ubingwa msimu huu katika Ligi Kuu Bara sababu tu ina kocha bora na mwenye uwezo.

 

Yanga kwa sasa inafundishwa na kocha Mkongo, Mwinyi Zahera ambaye ni rafiki mkubwa wa kocha Ibenge na wanafanya kazi pamoja katika timu ya DR Congo na wanaishi mtaa mmoja Ufaransa.


“Yanga safari hii watafanikiwa kutwaa ubingwa wao wa ligi kuu sababu wana kocha bora ambaye yuko makini na kazi yake na ninamfahamu vyema na hilo halinipi shaka hata kidogo.

 

“Sababu Zahera ni mtu wa kazi na analielewa vyema soka, hivyo sina wasiwasi naye katika hilo naona hata timu yake nafasi iliyopo kwa sasa katika ligi, wanaongoza kutokana na ubora wa mwalimu waliyenaye.

 

“Na sioni sababu ambayo itamfanya ashindwe kutwaa ubingwa mpaka hapo alipofikia sasa, yule ni rafiki yangu namfahamu vyema hata katika utendaji wake wa kazi,” alisema Ibenge ambaye ni rafiki mkubwa wa Nicholas Anelka wa Ufaransa.

Comments are closed.