Video: Machangudoa Walivyokamatwa Sinza Usiku Mnene, Wajitetea – DC Awaweka Ndani
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko akiwa na timu yake wiki hii wameendelea na oparesheni ya kushtukiza katika eneo la Sinza Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia June 15,2024 kwa lengo la kuyabaini na kuyafungia maeneo yanayotumiwa na machangudoa kuuza miili yao (Madanguro) ambapo wamefanikisha kukamatwa Watu 30 wakiwemo Madada poa 25 pamoja na Wateja wao watano.
DC Bomboko amesema “Makaka poa na Madada poa, Mashoga na Wasagaji wote hawana nafasi katika Wilaya ya Ubungo na wote wanaofanya biashara hizi warudi wakafanye shughuli nyingine, naagiza hawa wote waende kituo cha Polisi na baada ya Sikukuu wapelekwe Mahakamani na nielekeze oparesheni iwe endelevu maeneo yote, Watendaji wa Mitaa na Kata, Maafisa Tarafa na Polisi Kata na wengine Mimi nawaonesha mfano wajibu wa kupambana na Makahaba ni wa kwetu sote”