The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Manchester United Walivyoichapa Celta Vigo 0-1 (Europa)

0

Klabu ya soka ya Manchester United usiku wa kuamkia leo imechomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Celta Vigo katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Euefa Europa Ligi.

Goli pekee la Man U limewekwa kimiani na mshambuliaji kinda anayekuja kwa kasi Marcus Rashford mnamo dakika ya 67 kipindi cha pili cha mchezo.

Baada ya mchezo huo Timu hizo zitarejeana tena Alhamisi wiki ijayo huko Old Trafford Maskani ya Manchester United.

Akimzungumzia Rashford, Kocha wa Man U, Jose Mourinho amesema kuwa, kijana huyo ni mdogo kwa kwa maana ya umri wa miaka 19, mi kijana ambaye anapenda mpira, kila akimaliza mazoezi na wenzake anabaki uwanjani kwa dakika 30 kupiga free-kicks kila siku ili kujinoa zaidi.

Leave A Reply