The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Manji Ajisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi – Dar

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amejisalimisha kituo Kikuu cha Polisi (Central)  kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda aliyewataka watu wanaodaiwa kujihusisha na matumizi au biashara ya madawa ya kulevya kufika kituoni hapo kwa mahojiano.

Manji alifika kituoni hapo akiwa ameongozana na wanasheria wake nane. Licha ya kutakiwa kufika kituoni hapo Ijumaa, Manji alijisalimisha Alhamisi na baadaye, yeye na Askofu Gwajima waliondolewa kituoni hapo na gari jeupe kuelekea kusikojulikana.

Suala hilo limeleta mtikisiko mkubwa kwa mashabiki wa Yanga ambao hawajui hatima ya kiongozi wao huyo.
Tazama jinsi Manji alivyojisalimisha mwenyewe sakata la madawa ya kulevya kituo kikuu cha polisi kuitikia wito wa Makonda.

Comments are closed.