Video: Mapokezi ya Diamond Kigoma, Haijawahi Kutokea!
Mwanamuziki Diamond Platnumz amepokewa na mabango wakati akiwasili stesheni ya Nguruka Mkoani Kigoma katika kuadhimisha miaka yake kumi katika muziki.
Umati wa watu umejitokeza katika stesheni ya Nguruka Mkoani Kigoma wakiwa na mabango yaliyobeba jumbe mbalimbali kwa mwanamuziki huyo.
Moja ya mabango hayo lilikuwa limeandikwa “Karibu Diamond kwenu Kigoma tuijenge Kigoma, Sisi Nguruka tulishaanza ujenzi wa madarasa saba na vyoo 12. Tunaomba tuunge mkono, watoto 494 hawana pakusoma.”
Diamond aliyeanza safari ya kuelekea Kigoma jana Desemba 28, 2019 akiwa na mashabiki wake katika treni lengo lake kubwa ni kujumuika na watu wa mkoa huo kusheherekea miaka kumi tangu kuanza muziki.
Nguruka ikiwa ndio stesheni ya kwanza unapoingia Mkoa wa Kigoma, Diamond alikutana na umati wa watu ukimsubiri.
Baada ya kuwasili eneo hilo Diamond alipanda jukwaani na kuanza kuwaimbisha wakazi hao wimbo wa Baba lao.