Video: Mazishi ya Mwandishi wa Kituo cha Al Jazeera, Shireen Abu Akleh, Jerusalem

Mwandishi habari mashuhuri wa kituo cha televisheni cha Al Jazeera, Shireen Abu Akleh, anazikwa leo katika makaburi yaliyoko karibu na Mji Mkongwe wa Jerusalem, siku mbili baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi wakati akiripoti katika msako wa jeshi la Israel.

Mwili wa Shireen, raia wa Palestina na Marekani, umehamishiwa kutoka kwenye Ukingo wa Magharibi na mazishi yake yatafanyika katika kanisa la Jerusalem.

Israel na Palestina zimetupiana lawama kuhusu mauaji ya Shireen, aliyekuwa na umri wa miaka 51, na akifanya kazi katika Idhaa ya Kiarabu. Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa zimeunga mkono wito wa kufanyika uchunguzi kamili kuhusu kile ambacho Al Jazeera imekiita mauaji ya kukusudia.

 

Hata hivyo, Mamlaka ya Palestina imekataa kushirikiana na Israel kwenye uchunguzi huo, inayoituhumu kwa mauaji hayo.706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment