The House of Favourite Newspapers

Video: Mazishi Ya Mzee Mrema Kijijini Kwao Moshi, Umati Wafurika, Vilio Vyatawala

0

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha TLP, Augustino Mrema umezikwa Alhamisi Agosti 25 katika kijiji cha Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Maziko hayo yatatanguliwa na ibada ya mazishi siku ya Jumatano itakayofanyika katika kanisa Katoliki Parokia ya Salasala kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa na wastaafu wamefika kuhitimisha safari ya mwanasiasa huyo mkongwe nchini.

Baadhi ya viongozi hao ni Waziri Mkuu mstaafu John Malecela, Mbunge wa zamani wa Moshi Vijijini, Thomas Ngawaiya.

Wengine ni, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene anatarajiwa kumwakilisha Rais wa wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mrema.

Pia enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Leave A Reply