The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mary Mwanjelwa Atoboa Siri Mbili Sakata la Mchanga wa Madini

0

DODOMA: Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa ametoboa siri kuwa chanzo cha kuibiwa kwa madini kupitia kwenye michanga inayosafirishwa na wawekezaji kwenda nje kwanza ni mikataba mibovu ya uendeshwaji wa miradi hiyo na wawekezaji na pili ni viongozi kukoswa uzalendo.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma leo, Mwanjelwa amesema kuwa sababu hizo ndizo zimepelekea Taifa kupoteza kiasi kikubwa cha madini kutokanaa na wawekezaji wa migodi ya madini nchini kuamua kufanya wanayoyafanya sasa hivi kwani mikataba yetu haiwabani.

Hivi karibuni Raisi wa Jamuhuri wa Tanzania, Dkt. Joh Pombe Magufuli aliunda Kamati Maalum ya Kuchunguza Kiasi cha Madini Kilichopo Katika Mchanga unaosafishwa kwenda nje ya nchi ambapo makontena 277 yalichunguzwa na kubainika kuwa na kiwango kikubwa cha madini ambayo serikali na taifa kwa ujumla linapoteza jambo ambalo lilimlazimu Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Wazir wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Mkurugenzi wa TMAA pamoja na kuivunja Bodi ya TMAA huku akiagiza viongozi wake wachunguzwe na kuchukuliwa hatua haraka.

VIDEO: Mary Mwanjelwa Atoboa Siri Sakata la Mchanga wa Madini

Leave A Reply