The House of Favourite Newspapers

VIDEO: MO DEWJI Afunguka “Hatutaki Wachezaji wa Majaribio, Goli 5 Ziliniuma”

UONGOZI wa Simba umewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Ahly ambao ni wa Ligi ya Mabingwa utakaochezwa Februari 12, Uwanja wa Taifa.

 

Simba inakumbukumbu ya kupoteza michezo yake miwili ya ugenini katika hatua ya makundi hivyo deni lao kubwa ni kufanikiwa kushinda katika michezo yake mitatu iliyobaki.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simba Sports Club, Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema malengo makubwa ya klabu ni kuona inafanikiwa kupata matokeo chanya.

 

“WanaSimba na Watanzania kama tutajitokeza kwa wingi siku ya jumanne nina imani tutawafunga Al Ahly na tukiwafunga tutakuwa na nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kufungwa bao tano katika mechi zetu za ugenini kumeniuma sana, lakini bado hatujakata tamaa tuna imani ya kufanya vizuri katika michezo yetu iliyobaki kikubwa sapoti ya mashabiki.

“Shabaha yetu ilikuwa kufika kwenye makundi na tumefanikiwa na shabaha yetu nyingine ni kutetea kombe la Ligi Kuu ili tuendelee kushiriki mashindano haya,” alisema.

 

Mwenyekiti wa Simba, Sued Mkwabi amesema kwamba “Simba ikifanya vizuri faida ni kwa nchi yetu kuweza kupata mwakilishi zaidi ya mmoja kwenye mashindano yajayo, muhimu Wanasimba na wasio Wanasimba wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu ambayo ndio inawakilisha nchi yetu kwenye mashindano ya kimataifa,”.

Simba wapo kundi D kwenye hatua ya makundi ambapo kinara ni Al Ahly akiwa na pointi nne akifuatia na AS Vita ambaye ana pointi tatu huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi tatu na JS Saoura wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi mbili.

Wapinzani wao Al Ahly wanatarajiwa kutia timu alfajiri ya kesho tayari kwa mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Comments are closed.