The House of Favourite Newspapers

VIDEO: MREMA, KUPINGA WATU WANAOMKASHIFU RAIS MAGUFULI

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema,  alizaliwa mwaka 1945, huko mkoani kilimanjaro katika kijiji cha Kilaracha kilichopo Moshi vijijini akiwa mzaliwa wa pili katika familia ya watoto watano ya Mzee Lyatonga Mrema.

Safari ya Mrema kwenye ulingo wa siasa ilianza mnamo mwaka 1966 baada ya kujiunga na chama cha mapinduzi CCM.

Miaka yake katika siasa amepata nafasi ya kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo mwalimu wa siasa katika wilaya mbalimbali nchini,Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo, na badaye kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hata hivyo hakikuwepo kwenye Katiba ya nchi.

 

Huyo ndiyo Agustino Lyatonga mrema, mbali na kujiengua kutoka chama cha CCM na kuhamia NCCR Mageuzi na badaye TLP Mrema hajawahi kuacha kulitumikia taifa kwa kile anachoamini kuwa kinalipata taifa manufaa ya kusonga mbele kimaendeleo.

Comments are closed.