VIDEO: Mwanamke Auawa Kikatili, Akutwa Uchi/Polisi Wafunguka

MWANAMKE  aliyetambulika kwa jina moja la Khadija amepatikana akiwa amefariki maeneo ya Sinza-Afrika Sana, jijini Dar es Salaam,  akiwa hana nguo zozote mwilini (uchi).

Baadhi ya mashuhuda ambao wamefanikiwa kushuhudia tukio hilo wamefunguka na kusema kuwa wamemkuta ametupwa hapo tangu asubuhi ambapo watu walikuwa wakimpita kwa mshangao na kuondoka.

Hata hivyo,  hatimaye  polisi wa eneo hilo walipata taarifa na kufika eneo la tukio ili kufanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo ambapo waliuchukua mwili huo na kuupeleka hospitali ya Mwananyamala.


Loading...

Toa comment