Video: Mwenyekiti Tume Ya Uchaguzi Azungumza Kuelekea Uchaguzi MkuuTume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), imesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa kuzingatia katiba ya nchi, kanuni na utaatibu unaosimamia uendeshaji uchaguzi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Tume ta uchaguzi, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa NEC, uliowashirikisha wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Jaji Kaijage, amefafanua NEC itahakikisha uchaguzi unakuwa huru, wazi, haki na mazingira sawa ya ushindani kwa wagombea wa vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki.

Kuhusu vifaa vya uchaguzi, amesema tume inaendelea na ununuzi wa vifaa, ikiwemo uchapishaji wa nyaraka, vifaa vya elimu ya mpiga kura na karatasi za kura.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Toa comment