The House of Favourite Newspapers

Video: Polepole Awanaga Wapinzani Kutoshiriki Uchaguzi

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole,  leo Novemba 13, amevishambulia vyama vya upinzani vilivyotangaza kutoshiriki uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika  Novemba 24, 2019 na kusizitiza kwamba chama chake kitashiriki kama ilivyopangwa.

Ameyasema hayo wakati akiongea na na wanahabari  katika ofisindogoza CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam ambapo alisisitiza kwamba:

“Wapinzani wameogopa aibu, wameshajua hawatoshinda ndiyo maana wamegoma hata kukata rufaa, hata ukiwafuatilia katika mikutano yao hawana msimamo  na hawana kingine cha kusema.”
Aliongoza kwamba hapo nyuma kulikuwa na hatua za kusuasua kutoa fedha ya kuwawezesha wananchi, lakini katika awamu ya tano zimetenga zaidi ya Sh. bilioni 50 na imetunga sheria kwamba fdha hiyo ni  lazima wapewe wanawake, vijana na walemavu, jambo ambalo wananchi wanaliunga mkono kwa wingi.
“Sisi ndiyo chama pekee wenye ilani ya chama inayotekelezwa, hata katika uchaguzi wa serikali za mitaa tumeandaa ilani ndogo ambayo itakuwa na mambo ambayo tutawaahidi Watanzania na tutayatekeleza,” alisema na kuongeza kwamba  CCM kimeweka  uzito mkubwa katika uchaguzi huu kwa sababu mambo ya maendeleo ya wananchi yanaanzia ngazi ya serikali za mitaa, na ili safu ya uongozi wa juu ikamilike inaanzia chini na safu isipokamilika kunakuwepo na wizi na ubadhirifu katika fedha za umma.
Akizidi kusifia mambo yanayofanywa na chama chake alisema:  “Chama Cha Mapinduzi tunaingia katika uchaguzi huu tukiwa timamu na ili kupata watu sahihi watakaoweza kumsaidia Mheshimiwa Rais Magufuli kusimamia miradi yetu ya maendeleo na kuijenga nchi yetu.
“Hoja moja ambayo wapinzani wameitoa ni kuwa itungwe kanuni mpya ya uchaguzi.  Sasa tunawauliza wakati tunatunga kanuni hizi pamoja na wao,  walikuwa wamelala?” aliuliza na kuongeza:
“Kitendo cha mtu mzima kama Prof. Lipumba kunitusi na kunibeza kwamba ninaongozwa na njaa ambayo imenipanda kichwani si kitendo cha uungwana hata kidogo, anayejua nina njaa ni mke wangu peke yake na si mtu mwingine.
“Wale wote wanaonituhumu kuwa nimebadili msimamo wa kutetea mambo mbalimbali ikiwemo katiba (ya Warioba) huku wakidai njaa ndiyo imenibadilisha,  nataka niwaambie kuwa sijawahi kukana kauli yoyote niliyowahi kuisema na anayejua kuwa mimi nina njaa ni mke wangu pekee.”

 

Comments are closed.