Polepole: Mgombea Anawaambia Polisi ‘Nipigeni Risasi’ – Video

KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole, leo Oktoba 17, amezungumza na wanahabari na kutoa tathmini ya kampeni zao kuelekea Oktoba 28, siku ya uchaguzi mkuu mwaka huu 2020.

 

Kumekuwa na kauli za uchochezi, mgombea urais wa chama cha Zitto kabwe kule Zanzibar aliwaambia wafuasi wake wachukue mapanga na mawe wawe tayari, leo tunavyozungumza wana CCM wamevamiwa na kupigwa na kuumizwa kule Pemba.

 

“Leo tunavyozungumza hapa, kuna wana-CCM wamevamiwa, wakapigwa na kuumizwa Visiwani Pemba, hii ni siku moja baada ya mgombea Urais wa ACT-Wazalendo kusimamishwa kampeni kwa siku tano.

 

“Kabla ya kupiga kampeni CCM ushindi wake haupungui 75% na kamati ya ushindi ilikuwa imejiwekea malengo ya kura za urais ni 90%, unagundua Magufuli alianza ukanda mmoja, tukachukua makada waandamizi wakaenda upande mwingine.

 

 

“Tumekubaliana kila wanachama watatu wa CCM watuletee mtu mmoja, kutoka kwenye idadi ya wanachama wote milioni 17 wakifanya hivyo, tutapata kura za ziada milioni 5, ukijumlisha na milioni 17 unapata milioni 22. Kwa idadi tu ya wana CCM wenyewe tuna ushindi wa 75%.

 

“Asilimia 89 ya mikutano yote aliyoifanya Magufuli ameifanya asubuhi, angefanya jioni kama wenzetu ingekuwaje na mikutano yote imekuwa inasheheni watu katika namna ambayo hatukuwa tunategemea, nidhamu ya hali ya juu.

 

“Mgombea wa chama cha Freeman Mbowe na anayelinda maslahi ya mabeberu, yeye amekuwa akisema jamani mjiandae kuandamana nchi nzima, najiuliza hivi baada ya kampeni sheria inasema nini? Sheria inasema ukipiga kura rudi nyumbani, anawaambia polisi nipigeni risasi. Anayevunja sheria hapigwi risasi, unaandaliwa utaratibu anakamatwa na kuhukumiwa. 

 

“Halafu ni wepesi sana kuchukua tuvideo, wanakata ili kuondoka mantiki na kuvisambaza na kusema tumeonewa, nimewasikia watu jana wanasema eeh kuna mbunge msaidizi wake kakamatwa na polisi kavideo kanasambaa halafu wanalalamika.

Toa comment