The House of Favourite Newspapers

VIDEO: PSPF YAFUNGUA OFISI MPYA PEMBA NA UKEREWE, NI SEHEMU YA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

0


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

 

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza leo Oktoba 2, 2017.

“Mtakumbuka kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”
Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”

Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya, hapa makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.

Aliwataja washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu, (MCB).

Alisema, PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.
Miongoni mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na maafisa wa PSPF.

“Kwa kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa uchapakazi wa namna hii.” Alisema Dkt. Msengi.

Leave A Reply