The House of Favourite Newspapers

Infinix Wazindua Promotion Na Note 7

0
Meneja Masoko wa Infinix, Asajile Mwakasege akizungumza kwenye promosheni hiyo.

Kampuni ya simu janja za mkononi ya Infinix imezindua promosheni ya simu zake ikiwemo toleo lake jipya la Note 7 ambapo mnunuzi wa kipindi hiki cha promosheni ataweza kujipatia zawadi mbalimbali kwa kununua simu hizo kwenye maduka maalum ya promosheni hiyo. Promosheni hiyo itaendeshwa mikoa mbalimbali kwenye maduka maalum yaliyoteuliwa.

Wahudumu wa wateja wakionesha moja ya Tv, zinazotolewa kwa washindi wa promosheni hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni hiyo iliyofanyika jengo la China Plaza lililopo Kariakoo, Dar, Meneja Masoko wa Infinix, Asajile Mwakasege amesema kwa mteja atakayenunua simu hizo ataondoka na zawadi mbalimbali.

Mmoja wa wahudumu akimuonesha mteja ubora wa Infinix Note 7.

Katika uzinduzi huo ameuelezea ubora wa simu yao mpya aina ya Note 7 ambayo ina ubora wa hali ya juu na kuleta mapinduzi ya ubora katika simu janja zilizotangulia.

 

Amezitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na Tv ya flat skrini, mabegi ya kisasa, vikombe, chupa za kuifadhia vimiminika, pasi na nyinginezo.

Baadhi ya zawadi zinazotarajiwa kutolewa.

Asajile amesema katika kipindi hiki cha promosheni hakuna mteja yeyote atakayeinunua simu ya Infinix na kukosa zawadi japo ya kikombe ambacho hatakama hukujishindia zawadi kubwa hicho utapewa bure. Alisema Meneja Asajile.

HABARI/PICHA: WAANDISHI WETU      

Leave A Reply