VIDEO: SIKU 18 ZA KIFO CHA NAOMI, FAMILIA IMEAMUA HAYA!

IKIWA ni siku takribani 18 zimepita, tangu igundulike kuwa mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Hamis, amemuua mkewe, Naomi Marijani, na kisha kumchoma moto na majivu yake kuyafukia shambani kwao Mkuranga…

Familia ya Marehemu Naomi, imeandaa hafla maalum ya shukrani kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea huku wakiwa bado na majonzi makubwa ya kumpoteza ndugu yao huyo ambaye awali kabla ya kufahamu kuwa ameuawa na mumewe, walimtafuta kwa takribani miezi miwili.

Mume wa Naomi, ambaye ndiye mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya mkewe, bado anashikiliwa na jeshi la polisi huku kesi yake ikiendelea kuunguruma katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.


Loading...

Toa comment