The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Walichokizungumza Mwigulu, Lowassa Mazishi ya Nkaissery Kenya

0
Edward Lowassa.

 

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba wamehudhuria mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Jenerali Joseph Nkaissery aliyefariki ghafla Julai 8, mwaka huu ambapo viongozi hao wamepata fursa ya kuwahutubia wananchi wa Kenya wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu.

 

Akizungumza wakati wa hotuba yake, Lowassa amesema alimfahamu Jenerali Nkaissery tangu miaka ya nyuma ambapo alishirikiana naye kwa mambo mengi hususan ya kabila la Wamaasai.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba.

 

 

 

HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, MWIGULU NCHEMBA

HOTUBA YA EDWARD LOWASSA

 

Mbali na hivyo, Lowassa amemuelezea Nkaissery kuwa ni moja kati ya viongozi shupavu walioipenda na kuitumikia Afrika Mashariki, kuhakikisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapatikana na pia alikuwa mlezi mzuri wa amani.

 

Aidha, Lowassa amewaasa Wakenya kuendelea kuwa wamoja ili yasijirudie machafuko ya mwaka 2008 ya vita vya makabila vya wao kwa wao.

 

 

 

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba aliyeko nchini Kenya kwenye mazishi hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ametoa salamu za pole kwa Wakenya kutoka kwa Rais Magufuli huku akieleza kuwa nchi hiyo imepoteza mtoto na mtumishi aliyetukuka huku akisisitiza kuwa jambo hilo limeigusa sana Tanzania.

 

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Jenerali Joseph Nkaissery enzi za uhai wake.

 

“Tanzania haiwezi kuwa salama kama Kenya haiko salama, tumefanya naye kazi kwa pamoja kuhakikisha raia wa nchi hizi wanakuwa salama pamoja na mali zao. Mungu aendelee kuwagusa zaidi muendelee kustahimili kwani ni jambo ambalo halizoeleki.

“Tuwekeze kwenye utu wema kwani ni jambo jema kuliko utajiri wala kitu kingine. Tujifunze kwa Nkaissery,” alisema Mwigulu.

FUATILIA LIVE MAZISHI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA KENYA, JOSEPH NKAISSERY

Leave A Reply