Video: Waziri Mwigulu Awasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi

WAZIRI wa fedha, Dkt Mwigulu Nchemba, leo Juni 10, amewasilisha taarifa ya hali ya uchumi ya taifa ya mwaka 2020, ambapo baadae majira ya saa 10 atawasilisha bajeti kuu ya serikali bungeni.

 

Mwigulu Nchemba amesema, deni la Taifa, limeongezeka kwa Sh. 5.4 trilioni, kutoka Sh. 55.5 Aprili 2020, hadi Sh. 60.9 trilioni, Aprili 2021. Deni la nje ni Sh.43.7 trilioni huku la ndani ni Sh. 17.3 trilioni.

 

“Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani imeendelea kuwa tulivu ambapo dola 1 ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa Sh.2,298.5 Aprili 2021, ikilinganishwa na wastani wa Sh. 2,291.3 Aprili 2020.” amesema MwiguluTecno


Toa comment