VIDEO YA HARMONIZE & SARA MAHABA LIVE, WOLPER TABU IKO PALEPALE

Msanii kutoka WCB,  Harmonize na mpenzi wake Sarah (Mzungu) wameachia kipande cha video inayowaonyesha wakicheza kwa mahaba wimbo mpya wa ‘Paranawe‘ ambao ni wa Rayvanny pamoja na Harmonize.

 

Kipande hicho cha video kimewekwa mtandaoni na Harmonize mwenyewe pamoja na demu wake huyo ikiwa ni siku chache baada ya kuripotiwa kuwa wamemwagana kisha kurudi kwa mpenzi wake wa zamani, Jackline Wolper.

 

Tetesi za Harmonize kumpiga chini Sarah zilikuja baada ya Wolper kuonekana na kidume huyo kwa muda mrefu kwenye shoo ya Wasafi Festival Mtwara.

 

Harmonize anafanya vizuri na wimbo wake mpya walioutoa pamoja na Rayvanny unaoitwa, ‘Paranawe

ITAZAME VIDEO YA HARMONIZE WAKICHEZA NA SARAH

Toa comment