The House of Favourite Newspapers

Video ya Ngono ya Waziri Yanaswa, Atakiwa Kulipa Sh. Mil. 700

Image result for Malusi Gigaba

WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba, ametakiwa na mtu asiyejulikana kutoa Rand milioni tano (Sh. mil. 700) ili video ya ngono inayomwonyesha isisambazwe.  Video hiyo ilinaswa muda mfupi baada ya Gigaba kuteuliwa waziri wa fedha.

 

Hata hivyo, yeye amesema kuvuja kwa video hiyo ya ngono ni jaribio la kisiasa la kumchafua hususan sasa ambapo chama chake cha ANC kinatayarisha orodha ya watu watakaogombea ubunge katika uchaguzi ujao.

 

“Mke wagu na mimi tumesikitishwa na video hiyo ya ngono ambayo tulikuwa tuione sisi wawili tu kwani mawasiliano yangu ya simu yalidukuliwa mnamo 2016/17 na sasa inazungushwa miongoni mwa wanasiasa.

Image result for Malusi Gigaba

“Nachukua fursa hii kuomba msamaha kwa watu wengine wa familia yangu, hususan wanangu, mama yangu na wakwe zangu na wananchi wa Afrika Kusini kwa matatizo yatokanayo na jambo hili,” amesema Gigaba.

 

Katika video hiyo ya sekunde 13, Gigaba yuko peke yake akichezea uume wake kwa mkono na akisema: “Fikiria hiki kingekuwa mdomoni mwako.”

 

Wakati huohuo, Vuyo Mkhize msemaji wa Gigaba, amesema waziri huyo anasakamwa ili kuichafua njia yake ya kisiasa katika chama chake cha ANC na kwamba mara ya kwanza Gigaba kuifahamu video hiyo ni pale alipoteuliwa kuwa waziri wa fedha na Rais Jacob Zuma.

 

Pamoja na suala hilo kuripotiwa polisi, hawakuweza kufungua kesi kwa vile hawamjui aliyepiga simu hiyo ya vitisho.

LIVE: MWILI WA ISACK GAMBA UKIAGWA MUDA HUU

Comments are closed.