The House of Favourite Newspapers

Vifo Vyazidi Kuongezeka Mlipuko wa Volkano Guatemala – Pichaz

IDADI ya vifo vilivyotokea kutokana na Mlipuko wa Volcano ulioikumba Guatemala, imefikia watu 65 hadi sasa huku vikosi vya uokoaji vikibaini miili zaidi kutoka katika vijiji vilivyopo chini ya mwinuko wa eneo la Fuego lililokumbwa na Volcano hiyo na bado idadi kubwa ya watu hawajulikani walipo hadi sasa.

 

Taarifa zinasema kuwa zaidi ya watu 4,000 wameokolewa kutoka eneo la Kusini Magharibi mwa Guatemala, umbali wa kilomita 35 ambalo limeathirika na moshi wa Volcano hiyo pamoja uji wa lava. Watu milioni 1.7 ambao ni zaidi ya asilimia 10 ya watu wote nchini humo wapo katika hatari kubwa ya kukumbwa na madhara ya Volcano hiyo.

 

Mratibu wa majanga wa eneo la Escuintla, Luiz Meléndez amesema kuwa maandalizi yanaendelea kuhakikisha kuna maeneo ya kutosha kuwahifadhi wahanga wa tukio hilo.

“Tathimini kwaajili ya kuandaa mazingira ya kuwahifadhi watu inaendelea, ambayo inazingatia pia masuala ya usalama na mahitaji muhimu ya kuwa nayo, ili wananchi wasipate shida pale watakapopelekwa katika eneo la hifadhi,” alisema Luis Melendez.

 

Jorge Luis Altuve ambaye ni mmoja wa waokoaji iliyopo milimani, amesema wameanza kushuka kutoka maeneo hayo ya mlimani baada ya kuanza kukumbwa na giza, hivyo kuhofia usalama wao pia.

 

 

Shirika la kukabiliana na majanga nchini Guatemala limesema kuwa mlima Fuego ulilipuka siku ya Jumapili, huku majivu hayo yakirushwa hadi kijiji cha El Rodeo na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa wa makaazi ya watu huku baadhi yao wakiteketea ndani ya nyumba hizo.

 

Rais wa taifa hilo Jimmy Morales amesema vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhali imetolewa na vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhali imetolewa. Hata hivyo ya watu hao waliokufa kati yao watatu ni watoto. Mlipuko wa Volcano hii unatajwa kuwa zaidi tangu ule uliotokea mwaka 1974.

 

Hata hivyo ushauri umetolewa kwa raia kuvaa vifaa vya kuzuia pua zao kutokana na moshi na majivu yanayoendelea kurushwa kutokana na Volcano hiyo.

Video zilizochapishwa na vyombo vya habari nchini zinaonyesha miili ikiwa imetapakaa juu ya lava na maafisa wa uokozi wakiwahuhudmia watu waliofunikwa kwa jivu.

 

Mwanamke mmoja ameeleza kwamba lava ilimwagika katika mashamba ya mahindi na andhani kwamba huedna watu zaidi wamefariki. Jumla ya watu milioni 1.7 wameathirika na mlipuko huo wa volkano, serikali ya Guatemala inasema.

Comments are closed.