The House of Favourite Newspapers

Vigogo Wahaha Kuficha Mali Zao

3

pombeRais John Pombe Magufuli.

Stori: Makongoro Oging’ UWAZI
DAR ES SALAAM: Kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali (DPP) kutaifisha mali za watu binafsi zenye thamani ya shilingi bilioni 11 zilizopatikana kwa njia isiyo halali, baadhi ya vigogo sasa wanahaha kuficha mali zao wakihofia kukutwa na fagio hilo.

TULIKOTOKA
Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), Biswalo Mganga alisema serikali imetaifisha mali na nyumba za watu waliokuwa na kesi za rushwa, ujangili, madawa ya kulevya ‘unga’ na usafirishaji wa binadamu.

Pia alisema vita hivyo vinaendelea kwa wale wote wanaojipatia au waliojipatia mali kwa njia haramu ambapo watakamatwa na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

IMG_1413Moja ya mjengo wanayomiliki.

CHANZO CHA KIJESHI
Sasa kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya jeshi la polisi makao makuu jijini Dar, baadhi ya vigogo na waliokuwa vigogo kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wameanza kuficha magari na mali zao zingine kwa kuzifunga biashara, kuzimilikisha kwa ndugu zao au kuziuza.

“Jamani nataka niwape ukweli kuhusu juzi serikali kutangaza kwamba wametaifisha mali za watu zenye thamani ya shilingi bilioni 11. Ni kweli kama alivyosema DPP. Lakini hali ni tete. Baadhi ya vigogo waliopata mali kwa njia zisizo halali, wanajijua, sasa wameanza kuficha mali zao.

01wToyota Surf

WAFUNGA BIASHARA, WAUZA MAGARI
“Kuna wengine walikuwa na biashara kubwa, wamefunga ofisi zao. Yupo mwingine alikuwa anamiliki malori ya mafuta, sasa anahaha kubadili majina ya umiliki ili yawe ya mjomba wake.”

USALAMA WA TAIFA
“Serikali inajua yote. Na ilichofanya sasa, imewamwaga jamaa wa Usalama wa Taifa pembe zote za nchi ambapo wameanza kazi kimyakimya ili kujua kigogo gani anamiliki nini na nini na wapi.”

ITAKAVYOKUWA
“Kila mtu mali zake zitapigiwa mahesabu na kulinganishwa na mshahara wake kwa mwezi. Kama itaonekana aliibia serikali, anapelekwa mahakamani, akishindwa kesi, mali zitataifishwa na serikali,” kilisema chanzo hicho.

1999_Toyota_RAV4_(SXA11R)_Cruiser_wagon_(2011-11-17)_01Toyota Rav 4.

Kikaendelea: “Wengi wanaohaha kuficha mali zao ni jamaa wa TRA, TRL na TPA. Kule ndiko kuna mwanya mkubwa wa wizi. Lakini pia bado kuna wauza unga, nao wengi wana mali za kutisha.”

HALI YA NCHI KWA SASA
“Hali ya nchi kwa sasa si kama zamani. Rais Magufuli anataka kila mtu ale au apate mali kwa jasho halali na si kudhulumu mtu au kuibia serikali.”

TUJIKUMBUSHE KWA DPP
Tukirudi kwa DDP katika mkutano wake na vyombo vya habari, alisema hatua hiyo ilifanikishwa kupitia kitengo cha kuharamisha na kufuatilia mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu kilichoanzishwa rasmi kwa ajili ya kushughulikia na kufuatilia mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu ili kuzitaifisha na kuzirejesha serikalini.

Suzuki-Sidekick-SportSuzuki Escudo.

Alisema katika kipindi hiki kitengo hicho kimepata amri kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania na mahakama za chini na kutaifisha magari ya kifahari, fedha taslimu, akaunti za benki na nyumba, vyote vikiwa na thamani hiyo ya pesa.

Alitoa mfano wa mali zilizotaifishwa ni kiwanja kilichopo jirani na eneo la Ocean Road ambacho pamoja na mmiliki kujenga nyumba na baadaye kubomoa, tayari ameshindwa kesi na kiwanja hicho sasa ni mali ya serikali.

Alitaja baadhi ya kesi ambazo tayari zimeshughulikiwa na mahakama kutoa amri ya wahusika walipe faini ni ile iliyokuwa ikimkabili raia wa Marekani, John Galant ya uhujumu uchumi (2015) na Jensen Mubarak, raia wa Qatar.

DPP alisema Galant amehukumiwa kulipa Dola za Marekani 30,000 (sawa na shilingi milioni 64.2) na Mubarak vivyo hivyo.

Kesi nyingine ilimhusu raia wa Kuwait, Hussein Mansour aliyekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na kobe 173. Pamoja na kifungo, amehukumiwa kulipa Dola za Marekani 24, 220 (sawa na shilingi milioni 54.10).

DPP Mganga pia alisema kuna gari la watu waliokutwa na hatia aina ya Toyota Surf lenye namba za usajili T 103 DER, limetaifishwa na serikali. Aidha, mkoani Tanga katika kesi ya uhujumu uchumi, kuna magari mawili aina ya Toyota Rav 4 na Suzuki, yote mapya, yametaifishwa na serikali (angalia ukurasa wa mbele). Dar es Salaam kuna magari matatu (hakuyataja majina).

3 Comments
  1. Mama Juma says

    Bado mnagusa nyama tu. Noeni visu mfikie na mifupa.

  2. senator says

    Jipu ni katiba tunataka katiba itakayoleta uadilifu kwa Rais kutoshiriki,kuhusika kwa mamlaka yake kutoa amri ya kusababisha hasara kwa taifa,kwa misamaha holela ya kodi,na kukodisha au kuhodhi ardhi yetu kwa maslahi yake
    na washirika wake,Azimio la Arusha lifufuliwe,Mheshimiwa Rais Magufuli rudisha katiba ya wananchi,ila suala la muungano liwe serikali moja, sio tatu wala mbili,maana muungano ni kuunganisha na kuwa kitu kimoja.
    Rais ashtakiwe akifanya makosa akiwa madarakani,mkikataa hili majipu yatakuwa kansa.

  3. KIJUU says

    Ni furaha sana kusikia watu wasio na hofu ya Mungu wanashughulikiwa ipasavyo.Lakini mimi naona katika kutumbua majipu,kuna majipu mengine yamejificha na yapo sehemu nyeti,tunaomba hayo nayo yatumbuliwe ipasavyo na kusafishwa miji yao ili yasirudie tena.

Leave A Reply