Vigogo Waliopigwa Chini, Ubunge CCM Hawa Hapa!

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), jana Agosti 20, 2020, kimetaja majina ya wanachama wake wake watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang;anyiro cha kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao  Oktoba, huku baadhi ya  waliokuwa wabunge wake kipindi kilichopita wakitupiliwa mbali.

 

Awali mapema jana  akifungua Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt ajohn Magufuli, alisema kwamba vikao vyote vimepitia kwa kina majina hayo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wale watakaopitishwa ni wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya wananchi na chama kiujumla, huku akiwasisitiza wajumbe kuweka kando ukabila, ukanda na urafiki.

 

Majina yaliyopitishwa na kikao cha NEC, yalitangazwa mapema mchana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Hamphrey Polepole, na kwa asilimia kubwa ya mawaziri na wabunge waliokuwepo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wameteuliwa kuwania tena nafasi zao, huku wachache wakitupiliwa mbali.

 

Miongoni mwa waliopigwa chini  ni pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola; Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe;  aliyekuwa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga; aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa; Andrew Chenge na Prof. Jumanne Magembe.

 

Wengine ni pamoja na Dalali Kafumu, Dk. Charles Tizeba, Dk. Raphael Chegeni, Dk. Mary Nagu, Dk. Shukuru Kawambwa, Dk. Pundenciana Kikwembe, Profesa Noman Sigalla, Balozi Rajab Adadi, William Ngeleja, Peter Serukamba, Charles Kitwanga, Steven Masele, Omary Mgumba.

 

Baadhi ya majina ‘makubwa’ ambayo yanaingia kwenye kinyang’anyiro kwa mara ya kwanza ni pamoja na Hamis Taletale (Babu Tale), Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, Dkt. Tulia Ackson, Josephat Gwajima, Abbas Tarimba, George Ngassa, Festo Sanga na Eric Shigongo.

 

Watu wengine maarufu ambao walitia nia lakini hawajachaguliwa na chama hicho, ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda; aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema; aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri;  Peter Lijualikali, na Dkt. Vincent Mashinji, Abdallah Mtolea, Maulid Mtulia na wengine.

 

WABUNGE WA CCM WALIOPOTEZA UBUNGE WAO 2020

• Andrew Chenge – Bariadi Mashariki.
• Harrison Mwakyembe – Kyela
• William Ngeleja – Sengerema
• Peter Serukamba – Kigoma Kaskazini
• Raphael Chegeni – Busega
• Angella Kairuki – Same Mashariki
• Vick Kamata – Viti Maalumu
• Halima Bulembo – Viti Maalumu
• Charles Tizeba – Buchosa
• Adad Rajab – Muheza
• Diodorus Kamala – Nkenge
• Stephen Masele – Shinyanga Mjini
• Julius Kalanga – Monduli

• Maulid Mtulia – Kinondoni

•Lolesia Bukwimba – Busanda

•Juma Nkamia – Chemba
• Chacha Ryoba – Serengeti
• Albert Obama – Buhigwe
• Daniel Nsanzugwanko – Kasulu Mjini
• Mbaraka Bawazir – Kilosa
• Goodluck Mlinga – Ulanga
• Suleiman Saddiq – Mvomero
• Abadallah Mtolea – Temeke
• Haroon Pirmohamed – Mbarali
• Rafael Gashaza – Ngara
• Jumanne Maghembe – Mwanga
• Hassan Masala – Nachingwea
• Jitu Soni – Babati Vijijini
• Isaya Paulo – Mbulu Mjini
•James Ole Millya – Simanjiro
• Emmanuel Papian – Kiteto
• Omar Badwel – Bahi
• Issa Mangungu -Mbagala
• Augustino Masele – Mbogwe
• Venance Mwamoto – Kilolo
• Godfrey Mgimwa – Kalenga
• Mahmoud Mgimwa – Mufindi Kaskazini
• Edwin Sannda – Kondoa Mjini
• Charles Kitwanga – Misungwi
• Oscar Mukasa – Biharamulo Magharibi
• Pundenciana Kikwembe – Kavuu
• Richard Mbogo – Nsimbo
• Christopher Chiza – Buyungu
• Peter Serukamba – Kigoma Kaskazini)
• Noman Sigalla – Makete
• Kangi Lugola – Mwibara
• Deogratias Ngalawa – Ludewa
• Hassan Kaunje – Lindi Mjini
• William Dau – Nanyumbu
• Mary Nangu – Hanang
• Hasna Mwilima – Kigoma Kusini
• George Lubeleje – Mpwapwa
• Joel Mwaka – Chamwino
• Jerome Bwanausu – Lulindi
• Rashid Chuachua – Masasi
• Saul Amon – Rungwe
• Peter Lijualikali (Kilombero)

• Nimrod Mkono -Butiama
• Victor Mwambalaswa – Lupa
• Shukuru Kawambwa – Bagamoyo
• Haji Mponda – Malinyi
• Omary Kigoda – Handeni Mjini
• Mary Chatanda – Korogwe Mjini
• Mboni Mhita – Handeni Vijijini
• Edward Mwalongo – Njombe Mjini
• Joram Hongoli – Lupembe
• Greyson Lwenge – Wanging’ombe
• Dalali Kafumu – Igunga
• Mussa Ntimizi – Igalula
• Ezekiel Maige – Msalala
• Allan Kiula – Iramba Mashariki
• Justin Monko – Singida Kaskazini
• Janet Mbene – Ileje
• John Kadutu – Ulyankulu
• Anna Tibaijuka – Muleba Kusini
• Salum Khamis – Meatu
• Daniel Mtuka – Manyoni Mashariki
• Salum Khamis -Meatu Daniel
• Hamud Jumaa – Kibaha Vijijini.

 


Toa comment