The House of Favourite Newspapers

Vigogo Wapangwa Kukutana Robo Fainali FA Cup

0

DROO ya Robo Fainali imepangwa na sasa ni kama mambo yanaendelea kuwa matamu zaidi kw akuwa vigogo wengi wanatarajiwa kukutana katika hatua hiyo.

Everton yenyewe imepangwa kukutana na vinara wa Premier League, Manchester City.

Everton ilifanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kufunga Tottenham mabao 5-4 katika mchezo ambao ulitawaliwa na funga nikufunge.

Wabishi Leicester City wao wanatarajiwa kuwa nyumbani kukipiga dhidi ya Manchester United, mchezo ambao unaaminika utakuwa na ushindani mkali kwa kuwa tizo hizo hazipishani kwa kiwango cha juu katika msimamo wa Premier.

 

Bournemouth wanaoshiriki Championship wampangwa kukipiga dhidi ya Southampton wakati Chelsea itakuwa vitani na Sheffield United ambao wanashika mkia katika Premier League.

 

Southampton waliingia hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolves, wakati Chelsea iliingia kwa kuiondosha Barnsley kwa bao 1-0.Michezo hiyo inatarajiwa kufanyika wikiendi ya Machi 20 na 21, mwaka huu.

LONDON,England

MBWEMBWE za YANGA Kuelekea MCHEZO Dhidi ya MBEYA CITY – “TUNATAKA POINTI 3”..

Leave A Reply