VIINGILIO MECHI YA SIMBA VS YANGA VYAANIKWA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio katika mchezo wa Watani wa Jadi kati ya Yanga Sc na Simba Sc vikiwa vimegawanywa katika makundi matatu ambapo kiingilio cha chini zaidi kitakuwa ni shilingi 7,000 kwa viti vya mzunguko.

Viingilio vingine katika mchezo huo utakaopigwa Jumamosi Februari 16 saa 11:00 jioni vitakuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP A na 20,000 kwa VIP B na C.

Toa comment