The House of Favourite Newspapers

Vijana ACT-Wazalendo Dar Wampa Tano Rais Samia

0
Rais Samia Suluhu Hassan.

NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuunda tume ya kuangalia namna ya kuboresha mfumo wa haki jinai nchini, kwa kuwa itasaidia kuondoa changamoto ya ubambikaji kesi kwa wananchi

Pongezi hizo zimetolewa Februari 3, 2023 na Mwenyekiti wa Ngome ya ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Kamugisha, ikiwa ni siku chache tangu Rais Samia azindue tume hiyo itakayofanya kazi kwa muda wa miezi minne kuanzia Februari hadi Mei mwaka huu.

“Januari 14, 2023, kupitia kongamano la vijana wa Dar es Salaam, niliibua tabia ovu ya askari wetu kubambikia vijana kesi. Ahsante Rais kwa hatua ulioanza nayo kuutazama mfumo wa haki nchini,” amesema Kamugisha.

Rais Samia ameiagiza tume hiyo ipitie upya utendaji wa taasisi za haki jinai, ikiwemo mahakama, Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), ili kubaini changamoto zinazopelekea zishindwe kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa ajili ya kuzitatua.

Leave A Reply