The House of Favourite Newspapers

Vijana Mwanza Watakiwa Kujiajiri

0

Wanachama wa Kikundi cha Wafanyabiashara na Watumishi wa Umma  Marafiki kutoka jijini  Mwanza maarufu Mwanza Friends Association wanaofanya shughuli zao kwenye mikoa mbalimbali nchini Tanzania wamewataka vijana kujiajiri ili kupunguza vijana ambao hawana ajira hapa nchini.

Akizungumza na Global Publishers, Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association, Patrick Joseph amesema kuwa; “Ni ukweli usiopingika kwamba hapa nchini kuna vijana wengi hawana ajira na wamesoma wana Elimu zao hivyo sisi kama vijana wenzao tunawasihi wajiajiri ili waache kuishi maisha tegemezi ya kutegemea ajira za serikalini ambazo hazijulikani zitatoka lini.

 

“Kikundi cha Marafiki kutoka Mwanza ‘Mwanza Friends Association’ chenye Makao yake Makuu Jijini Mwanza kinaundwa na Wafanyabiashara na Watumishi wa Umma wanaotoka Mkoa wa Mwanza lakini sasa wanaishi kwenye mikoa mingine nchini na sisi tuliamua kuungana ili kujenga umoja ambao utakua imara na wenye lengo la kuinuana kiuchumi kutoka kwenye Umaskini hivyo tunatamani vijana wenzetu watuige ili na wao waweze kuwa na biashara zao ili wafanikiwe kimaisha kuliko kutegemea ajira za serikalini ambazo haijulikani zitatoka lini na hata zikitokea sio wote watakao ajiriwa”, alesema Joseph.

 

“Sisi kama Mwanza Friends tuliamua kujisajili ili tutambulike kisheria na tayari tunayo katiba yetu na mpaka sasa tuko wanachama 35 ambapo kwa sasa tukihitaji mikopo sehemu yoyote tunaweza kukopa ili kuendeleza maisha yetu hivyo tunawaomba vijana wengine wachangamke kwa kuanzisha miradi mbalimbali ili waweze kufikia ndoto za  maisha yao sio kutegemea ajira za serikali na tunaamini hilo likifanyika malalamiko hayatakuwepo kwamba serikali haijatoa ajira”

Na Johnson James- GPL MWANZA

Leave A Reply