The House of Favourite Newspapers

Vijana Waitwa Kwenye Usaili na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Majina Yapo Hapa

0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura.

Mkuu wa Jeshi la Polisi anapenda kuwatangazia kuwa vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi kupitia mfumo wa Ajira TANZANIA POLICE FORCE RECRUITMENT PORTAL, usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 29/7/2024 hadi tarehe 11/8/2024 nchini kote.

Waombaji wa Tanzania Bara wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) kilichopo Barabara ya Kilwa (Kurasini).

Waombaji wenye elimu ya kidato cha nne na sita usaili wao utafanyika kwenye mikoa walioichagua wakati wa kutuma maombi.

Waombaji wa Zanzibar wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na nne usaili utafanyika Zanzibar. Kwa walioko Mikoa ya Unguja usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na Mikoa ya Pemba usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).

Kila mmoja anatakiwa kufika akiwa na vyeti halisi vya taaluma (academiccertificates), cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Mamlaka ya Utambulisho wa Taifa NIDA au namba ya utambulisho wa Taifa NIDA, nguo na viatu vya michezo.

Kijana yeyote atakaefika kwenye usaili baada ya tarehe 29/07/2024 hatopokelewa. Orodha ya vijana waliochaguliwa kufanya usaili imeambatishwa pamoja na tangazo
hili.

Imetolewa na;
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
S.L.P 961
DODOMA
22/07/2024.

Bonyeza hapa kuona >> ORODHA YA VIJANA WALIOITWA KUFANYA USAILI

SAMIA na SIKU 19 NZITO-KUKATWA kwa NAPE na MAKAMBA GUMZO-MATAPELI VIWANJA KUDAKWA-FRONT PAGE

Leave A Reply