Vijana Waliopotea Temeke Wafikia 4, Mochwari Na Polisi Hawapo – Video
Sakata la vijana wawili, Abdulrazack Salim na Ramadhan Sultan wakazi wa na Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam kudaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha, ndugu zao wakidai kwamba wametekwa, mapya yameibuka.
Wazazi wa vijana wengine wawili nao wamejitokeza na kueleza kuwa watoto wao walitoweka siku moja sawa na wale wawili wa mwanzo katika mazingira yanayofanana na kufanya jumla ya waliopotea kufikia vijana wanne.
Takribani siku 19 zimepita mpaka sasa bila vijana hao kuonekana.