The House of Favourite Newspapers

VILIO! Mwili wa Dada wa Shigongo Wawasili Bupandwamhela – (Pichaz + Video)

Mwili wa marehemu Vaileth ukitolewa nyumbani kwake, Nyamhongolo ili kuingizwa kwenye gari kwa safari ya Bupandwamhela.

MWILI wa dada wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, marehemu Vaileth James Bukumbi, umewasili leo Alhamisi, Juni 20, 2019, nyumbani kwao katika Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosa – Sengerema mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko.

Msafara wenye mwili ukiwa kwenye ferry ya kamanga tayari kwa kuvuka.

 

Msafara wa uliyokuwa na mwili huo kutokea maeneo ya Nyamhongolo, nje kidogo ya jiji la Mwanza alikokuwa akiishi marehemu, umepokelewa na umati mkubwa wa waombolezaji, ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wakisubiri kuupokea mwili wa ndugu yao mpendwa ambaye aliaga dunia usiku wa kuamkia juzi Juni 18, 2019 jijini humo.

Vilio, simanzi na majonzi vimetawala wakati wa kuupokea mwili huo  miongoni mwa waombolezaji wakiwemo watoto wake, dada zake, kaka zake na ndugu wote wa familia ya marehemu Mzee James Bukumbi.

Msafara ukielekea kijijini.

 

Mwili wa marehemu Vaileth unatarajiwa kuagwa na kuzikwa kesho nyumbani kwao Bupandwamhela ambako wazazi wake, Mzee James Bukumbi na Bi Asteria Kapera aliyeaga dunia Julai mwaka jana, wote wamezikwa hapo.

 

Shigongo akisalimiana na waombolezaji baada ya kuwasili nyumbani kwao.

 

Waombolezaji wakimpa pole Shigongo.

 

Mwalimu Elias Ndutu, akimpa pole Shigongo.

 

 

Dada wa marehemu (aliyeko mbele) na wifi wa marehemu ambaye ni mke wa Shigongo (mwenye nguo nyeupe) wakiwa wenye huzuni kumpoteza ndugu yao.

 

Mwili ukiwasili nyumbani.

 

Jeneza lenye mwili wa marehemu baada ya kuwasili nyumbani.

 

Waombolezaji wakiwa wenye huzuni.

 

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Global Digital, Edwin Lindege baada ya kuwasili msibani hapo.

 

Msanifu Kurasa wa Global Publishers, Glory Lucas akimpa pole Shigongo.

 

Mwandishi wa Global Publishers, Imelda Mtema akimpa pole Shigongo.

 

Mwandishi wa Gazeti la Spoti Xtra, Martha Mbona akimpa pole Shigongo.

 

Kaka yake na Shigongo aitwaye, Mtima Fundikira akimpa pole.

 

Shigongo akipeana pole na Baba Yake Mdogo, Mzee Zabron Bukumbi.

 

Mwili baada ya kuwasili.

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

TAZAMA HAPA VIDEO

Comments are closed.