visa

Vilio Upya Makaburini! Misa ya Wazazi wa Anna Zambi – Video

SIMANZI na majonzi vimeibuka tena leo Jumamosi, Novemba 30, 2019 katika familia ya Mwanafunzi Anna Zambi ambaye miezi michache iliyopita alifiwa na wazazi wake wote wawili pamoja na ndugu zake watatu.

 

Waalimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mama Teresa wa Culcuta ya Same, Kilimanjaro aliyokuwa akisoma Anna, wamefika eneo la Goba katika makaburi waliyopozikwa wazazi na ndugu wa Anna kwa ajili ya kufanya Ibada ya Misa ili kuwaombea na kubariki makaburi hayo.

 

Anna Zambi, aliyeondokewa na wazazi wake wawili na wadogo zake watatu katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Tanga.

 

Wazazi walikuwa wakifahamika kwa majina ya Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo zake watatu, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa wamepanda kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga.

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA
Toa comment