The House of Favourite Newspapers

Vilio Vyatawala Mtoto Aliyetekwa Akirudishwa, Mama Yake Afunguka – Video

Mama mzazi wa mtoto Merysiana Melkzedeck.

Vilio vizito vilitawala hapo jana, Januari 24, 2025 baada ya mtoto Merysiana Melkzedeck aliyekuwa ametekwa na wahalifu waliovamia nyumbani kwa wazazi wake na kupora mali mbalimbali ikiwemo gari, kurejeshwa kwenye mikono ya familia hiyo.

Mama mzazi wa mtoto amefunguka kupitia Global TV ambapo amekiri kuwa na furaha baada ya mwanaye kurejea akiwa mzima kabisa.