Vilio Vyatawala Mwili wa Makongoro Ukiwasili Kwake – Video

 

MWILI wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kichama wa Ilala Jijini Dar es Salaam, Dkt. Milton Makongoro Mahanga, umewasili nyumbani kwake maeneo ya Segerea jana kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika leo Machi 26, 2020.

 

Makongoro alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu, Machi 23, 2020 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu tangu juzi.

 

Dk. Makongoro kabla umauti kumfika alikuwa Mwenyekiti wa Chadema wilayani Ilala, awali alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Ukonga kisha Segerea.

 

Pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Naibu Waziri wa Miundombinu na Maendeleo, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kwa nyakati tofauti wakati akiwa mbunge katika serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kabla kuhamia Chadema. 

 

Toa comment