The House of Favourite Newspapers

VINARA Tusua Maisha Kuzawadiwa Kwenye Uzinduzi wa Spoti Xtra

WASHINDI wa droo ya 11 na 12 wa Shindano la Tusua Maisha na Global lililofikia tamati Jumanne ya wiki hii, wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao kwenye uzinduzi wa Gazeti la Spoti Xtra Alhamisi, unaotarajiwa kufanyika Alhamisi ya wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

 

Tangu kuanzishwa kwake, Desemba, 2017, Gazeti Bora la Michezo la Spoti Xtra, lilikuwa likitoka Jumapili pekee lakini kutokana na kiu ya wasomaji, sasa gazeti hilo litakuwa linatoka mara mbili kwa wiki, Alhamisi na Jumapili na katika uzinduzi wa toleo jipya, ndipo washindi hao watakapokabidhiwa zawadi zao.

 

Wanaotarajiwa kukabidhiwa zawadi zao ni Bolen Kilimba aliyejishindia pikipiki, Silvanus Nyombe wa Mwanza aliyejishindia dinner set na Eliuter Ndunguru wa Manyoni, Singida aliyejishindia jezi.

 

Wengine ni Halima Jabir wa Mbagala aliyejishindia pikipiki, Hadija Shaban, mfanyabiashara kutoka Morogoro aliyejishindia ada ya shule, Hamis Mohamed wa Kinondoni jijini Dar es Salaam aliyejishindia dinner set na Vaileth Mtilega wa Kiwalani aliyejishindia jezi.

 

“Tunahitimisha Tusua Maisha na Global lakini kwa wasomaji wa habari za michezo, tunakuja na ofa nyingine kabambe kwenye Gazeti la Spoti Xtra ambapo kwa kuanzia, tumeshusha bei kutoka shilingi 800 hadi shilingi 500, huku pia kukiwa na zawadi nyingine kemkem.

 

“Uzinduzi rasmi utafanyika Alhamisi na siku hiyo ndiyo tutakabidhi pia zawadi kwa washindi wetu wa droo mbili za mwisho. Nawasihi wasomaji wetu kuendelea kusoma magazeti ya Global Publishers kwani yajayo yanafurahisha,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja wa Global Publishers na kuongeza:

 

“Kwa wasomaji wa Spoti Xtra, kazi ndiyo kwanza imeanza kwani katika kila toleo tutakuwa tukitoa zawadi mbalimbali za michezo kama jezi za klabu mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

 

“Kwa kununua Gazeti la Spoti Xtra utapata namba maalumu kwenye kuponi iliyoko ndani ambayo utaelekezwa jinsi ya kutuma na kila wiki utakuwa ukishinda jezi ya klabu unayoipenda na mipira.”

Comments are closed.