The House of Favourite Newspapers

Vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga Yaitungua Dodoma Jiji 2-0 Uwanja wa Jamhuri

0

Yanga imeifunga Dodoma Jiji FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Ushindi huo umekuja baada ya kucheza mechi tatu mfululizo bila kushinda

Ni mabao ya Dickosn Ambundo dk ya 11 na bao la pili lilifungwa na kipa wa Dodoma Jiji,Mohamed Yusuph dk ya 35 katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Zawad Mauya jamo lililomfanya ajifunge.

Kinara wa mabao ndani ya Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa yeye kutokufunga sio tatizo kikubwa ni ushindi wa timu.


“Nimekuwa nikipata nguvu ya kuendelea kupambana licha ya mabeki kuweza kunikamia wakitaka nisiweze kutetema kwenye mechi ambazo wanacheza wanahitaji nisiteteme.

“Ushindi wa timu ni kitu cha msingi kisha mimi ninakuwa na kazi ya kutimiza majukumu yangu hasa kwa malengo ambayo ninakuwa nimejiwekea,” amesema.

Yanga inafikisha pointi 60 ikiwa imecheza mechi 24 ndani ya Ligi Kuu Bara aa haijapoteza mchezo mpaka sasa.
Kiungo wa Dodoma Jiji, Hassan Nassoro aliweza kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa dk ya 88 kwa kumchezea faulo Yannic Bangala.

Leave A Reply