Vinara wa ligi kuu England Arsenal Wachapwa na Everton bao 1-0
Vinara wa ligi kuu England Arsenal imelala kwa bao 1-0 dhidi ya Everton iliyokuwa nafasi ya pili kutoka mkiani katika mchezo wa mapema uliopigwa kwenye uwanja wa Goodson Park. Ni mechi ya pili Arsenal kufungwa msimu huu.
Arsenal iliingia ikiwa haijapoteza mchezo wowote katika michezo 13 iliyopita ya ligi huku Everton ikiingia ikiwa haijashinda katika michezo 8 iliyopita.
Katika mchezo uluomalizika punde, Everton chini ya kocha mpya anayeiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza, Sean Dyche ilionekana hatari zaidi ya Arsenal ambao leo makali yao hayajaonekana kabisa.
Goli pekee la Everton limepachikwa na mlinzi James Tarkowski kwa kichwa baada ya kona ya McNeil katika dakika ya 60 kushindwa kuzuiwa na mabeki wa Arsenal.
Pamoja na kufungwa bado Arsenal inaongoza ligi hiyo kwa alama 5, huku Everton ikipaa kwa nafasi mbili hadi nafasi ya 17 ikiwa na alama 18.