The House of Favourite Newspapers

VINARA WIZI WA MAGARI,  WATUHUMIWA 10 WA UJAMBAZI, WAKAMATWA DAR

Kamishna wa Polisi Kanda Dar es Salaam,SACP  Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).. 
…Mabosasa akiwaonesha bastola zilizokamatwa waandishi wa habari .

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 10 kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha pamoja na vinara wizi wa magari.

 

Kamishna wa Polisi Kanda  Maalum Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa, watuhumiwa hao ni Bushiri Ally (29) mkazi wa Tandika, Mohamed Ismaili (18) mkazi wa Tandika, Issa Saidi (19) mkazi wa Yombo, Mlekwa Ally (18) mkazi wa Tandika, Shabani Nassoro (17) mkazi wa Tandika, na watano wengine ambao majina yao yameyahifadhi kwa sababu za kiupelelezi.

 

Akifafanua zaidi, Mambosasa ameeleza kwamba mnamo Aprili 29, 2018 majira ya saa sita usiku huko maeneo ya Tandika Foma askari wakiwa doria walilitilia shaka gari namba T 401 CLF Toyota Alteza rangi ya fedha na kuanza kulifuatilia kisha kulikamata na kukuta watu watano wakiwa ndani ya gari hilo.

 

Baada ya hapo askari waliwaweka chini ya ulinzi watu hao na kufanya upekuzi ndani ya gari hilo na kufanikiwa kukamata Bastola aina ya BROWNING yenye namba N635BRE ikiwa na risasi mbili katika  Magazine yake.

 

Na Denis Mtima/Gpl.

Comments are closed.