The House of Favourite Newspapers

VINASABA VYAONYESHA WAINGEREZA WALIKUWA WEUSI!

Utafiti wa vinasaba unaonyesha hivi ndivyo Mwingereza wa zamani alivyokuwa. Alikuwa na ngozi nyeusi na nywele nyeusi zenye kujipindapinda. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika mabaki ya mifupa ya mtu yaliyoitwa Cheddar Man aliyefariki miaka 10,000 iliyopita. Mabaki hayo kaili ya binadamu ndiyo ya zamani zaidi kupatikana nchini Uingereza.

UCHUNGUZI  wa vinasaba (DNA) uliofanywa karibuni umeonyesha kwamba Mwingereza aliyeishi miaka ipatayo 10,000 alikuwa na ngozi nyeusi, macho ya bluu na nywele  nyeusi,  ndefu zenye kujipindapinda.

 

Utafiti huo ulitokana na mabaki ya fuvu na mifupa kamili ya binadamu aliyekufa miaka 10,000 iliyopita aitwaye Cheddar Man ambavyo vilichimbuliwa eneo la Cheddar Gorge, Somerset,  Uingereza, mwaka 1903 na ambapo mabaki hayo yanasemekana kuhusiana kinasaba na mtu mmoja kati ya kumi nchini Uingereza leo.

Mabaki kamili ya Cheddar Man yaliyofanyiwa utafiti.

Vipimo vilivyochukuliwa vinaonyesha kwamba asilimia 76 ya mtu huyo wa Cheddar, alikuwa mtu mweusi ambapo  inaonyesha pia kwamba wakazi wa visiwa vya Uingereza, walikuja kupata ngozi nyeupe baadaye kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Fuvu la Cheddar Man lililofanyiwa uchunguzi mkubwa zaidi.

Wakati wa Cheddar Man anafariki, idadi ya watu nchini Uingereza ilikuwa ni 12,000 ambapo vinasaba vya mtu huyo leo hii vimepatiana katika nchi zingine za Ulaya huko Hispania, Hungary na Luxembourg.

Waingereza wa leo wakijilinganisha na Mwingereza aliyekuwepo miaka10,000 iliyopita.

Wanasayansi wanasema pia kwamba  mababu wa Cheddar Man waliingia Uingereza kupitia Mashariki ya Kati baada ya kuondoka barani Afrika.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI

Comments are closed.