The House of Favourite Newspapers

Vini Atafungiwa Kisa Utovu Wa Nidhamu

0

 

Winga wa Timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Real Madrid, Vinicius Junior (24) huenda akakumbana na adhabu ya kufungiwa michezo isiyozidi sita na Shirikisho la Mpira wa Miguu Amerika Kusini, (CONMEBOL) endapo atakutwa na hatia ya kumtukana mwamuzi katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia ugenini dhidi ya Timu ya Taifa Venezuela.

Katika mchezo huo uliomalizika wa sare ya 1-1, mwishoni mwa mchezo huo katika dakika za nyongeza, Vini alionekana kumkaripia mwamuzi wa akiba na kumtamkia maneno kwa lugha ya kireno yaliyoashiria kumkebehi na kumtukana.

(CONMEBOL) bado haijatoa maamuzi yeyote hadi sasa, huku uchunguzi ukiwa unaendelea, na iwapo mchezaji huyo atakutwa na hatia yakumtukana mwamuzi huyo basi huenda akakutana na adhabu ya kufungiwa michezo minne hadi sita na kupigwa faini.

Katika mchezo huo, nyota huyo wa klabu ya Real Madrid alicheza dakika zote katika mchezo huo, na kushindwa kuiandikia timu yake bao baada ya kukosa mkwaju wa penalti dakika ya 62, huku goli la Brazili likifungwa dakika ya 43 na Raphinha kabla ya Talesco Segovia kuisawazishia timu yake mwanzoni kabisa mwa kipindi cha pili.

Leave A Reply